111 : 1
تَبَّتْ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ وَتَبَّ
Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. [1]
111 : 2
مَآ أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ
Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. [2]
111 : 3
سَيَصْلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ
Atauingia Moto wenye mwako. [3]
111 : 4
وَٱمْرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلْحَطَبِ
Na mkewe, mchukuzi wa kuni, [4]
111 : 5
فِى جِيدِهَا حَبْلٌ مِّن مَّسَدٍۭ
Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa. [5]